TABORA GIRLS; Na Jeshi la polisi Tabora
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Liberatus Barlow
MWALIMU mmoja wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Tabora (Tabora Girls) ya mjini Tabora, anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa akikabiliwa na tuhuma za kumbaka mwanafunzi wake asiyeona.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Liberatus Barlow, alisema mtuhumiwa huyo mwalimu Steven Pius (31), alimbaka mwanafunzi huyo (jina linahifadhiwa) majira ya saa 7 mchana, Septemba 19, mwaka huu katika ofisi ya shuleni hapo.
Alisema siku ya tukio, Pius alimwita mwanafunzi huyo anayesoma kidato cha nne na mwenye umri wa miaka 21, kwenye ofisi yake na kuanza kumshawishi kufanya naye mapenzi.
Kamanda huyo alisema mwanafunzi huyo alikataa kufanya mapenzi na mtuhumiwa na badala yake mtuhumiwa alitumia nguvu, ambapo alimvua nguo na kuanza kumbaka mwanafunzi huyo mwenye ulemavu wa macho.
Alisema baada ya mtuhumiwa kufanikisha kitendo hicho ambacho kilimsababishia binti huyo maumivu makali na kutokwa na damu nyingi sehemu za siri, alimuwekea sh 5,000 kwenye mfuko wa sketi yake kama kifuta jasho.
Wanafunzi walipohojiwa, walisema baada ya kufanyiwa tukio hilo aliondoka kuelekea bwenini, huku akilia na kwamba wenzake walipomuuliza jambo lililomsababisha kulia hakuweza kuwaambia, ingawa walishangazwa na damu iliyokuwa ikichuruzika.
Karibu katika ULIMWENGUWA BLOG.
ReplyDeleteBasi ndio kumekucha na tuendelee kuielimisha jamii kuhusiana na yale mema tutakayo na mabaya tupingayo
Baraka kwako na kwa wale wema wakusaidiao.
Blessings