PATA MATUKIO MBALI MBALI YA KIJAMII POPOTE ULIPO!

Friday, October 8, 2010

TUNATOA PONGEZI ZA DHATI KWA RAIS WETU MPENDWA NDUGU JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA KUWEZA KUTIMIZA MIAKA 60...

MIMI NIMKA LAMECK (11) MWENYEKITI WA CHIPUJKIZI WILAYA YA KINONDONI NA MWANAHARAKATI WA KUTETEA HAKI ZA WATOTO NCHINI NA MTANDAO HUU TIMU NZIMA YA 'HAKIMTOTO BLOG' TUNAKUPA ''TANO'  .... OKTOBA 7 SIKU YA JANA KIKWETE AMEWEZA KUTIMIZA MIAKA HIYO 60, SAMBAMBA NA HILO NI HAKIKA TUNAKUTAKIA KILA LA KHRLI KATIKA KAMPENI ZAKO NA KUSHINDA USHINDI WA KISHINDO.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata keki wakati wa sherehe ya kuadhimisha miaka 60 tangu kuzaliwa kwake pembeni yake ni Mama salma Kikwete na mjukuu wao Karima wakishuhudia.
Rais Jakaya Kikwete akimlisha keki mmoja wa wajukuu zake usiku wa kuamkia leo kwenye hafla ya kuzaliwa kwake iliofanyika katika viwanja vya taasisi ya WAMA.,kulia kwake ni Mama Salma Kikwete.
Rais Jakaya Kikwete akimlisha keki mkewe Mama Salma Kikwete usiku wa kuamkia leo,Mh Jk usiku wa kuamkia leo alikuwa anatimiza miaka 60.
Rais Kikwete na Mkewe mama Salma Kikwete wakitakiana afya njema kwa kucheeers mbele ya wageni waalikwa usiku wa kuamkia leo,Rais Kikwete alikuwa akisherehekea siku yake maalum ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka 60.
Mtoto wa Rais Kikwete,Ridhiwani Kikwete akimpa zawadi baba yake na pia kumpongeza kutimiza miaka 60 ya kuzaliwa kwake,kwenye hafla fupi iliofanyika usiku wa kuamkia jana katika viwanja vya taasisi ya WAMA na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali.
Mtangazaji mahiri wa Clouds FM,Eprahim Kibonde akimkabidhi jezi ya timu ya Taifa ya Morroco Rais Kikwete ambayo wameitoa kama zawadi kwake.Timu hiyo itacheza na timu ya Taifa,Taifa Stars hapo kesho katika uwanja wa Taifa jijini Dar.
Wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Prof Jay pamoja na Mwana FA wakizungumza jambo na Rais Kikwete na pia kumpa pongezi za dhati kabisa kwenye hafla hiyo iliyokuwa ya kuvutia usiku wa kuamkia leo.
Kwa picha zaidi tembelea http://www.michuzijr.blogspot.com/

Habari hizi ni kwa msada wa mtandao wa Mo blog na Michuzi blo.


 

No comments:

Post a Comment