PATA MATUKIO MBALI MBALI YA KIJAMII POPOTE ULIPO!

Monday, January 24, 2011

NDANI YA BILICANAS JANUARI 30..



Z.Anto amlilia ‘Binti Kiziwi’ Bilicanas

MSANII  nyota wa kizazi kipya nchini Ally Mohammed 'Z-Anto'  ama Malavidavi guru’ usiku wa kuamkia leo 24 na kuweza kumlilia ‘Binti Kiziwi’ na kufanya burudani kuwa ya kipekee  katika  ijulikanayo ‘Bongo Stars Nite’ inayofanyika kila jumapili jijini Dar es Salaam,ndani ya ukumbi wa kimataifa wa Club Bilicanas.

Katika shoo hiyo, Z.Anto aliweza kuimba ambamba na Pingu ambapo walipamba kwa freestyle mbalimbali sambamba na kuimba vibao vyao vinanvyotamba katika chati za Bongo kwa sasa na zamani.

Baadhi ya vibao hivyo ambavyo viliwadadtisha wadau wa burudani wliofurika ndabni ya Bilz ni pamoja na ‘Binti Kiziwi’ ambacho kiliweza kuwakonga wengi na kuamsha shamrashamra za mara kwa mara wakati msanii huyo alipokuwa akiingizia vionjo mbalimbali katika midundo (beat) ya kibao hicho na kufanya shoo kuwa na shangwe muda wote

Nyimbo nyingine walizowakonga nyoyo mashabiki ni pamoja na ‘Kisima cha Malavidavi’, ‘Sauti ya Deejay’, ‘Peace and Love’ na nyingine nyingi.

Pingu na Z.Anto  wamekuwa kwakishirikiana kwa ukaribu muda mrefu toka kutoa kibao hicho cha ‘Binti Kiziwi’ hali uyo imewafanya kuwa na mafanikio makubwa na kuweza kupiga shoo ndani na nje ya nchi wakiwapamoja.

Katika shoo ya wiki ijayo ya Januari 30, msanii nyota Steve RnB  ‘Loverboy’ akisindikizwa na Baby boy, watapishoo kali kwa vibao vikali vinavyotamba kama ‘Onelove’, ‘Sogea karibu’ na vingine vingi huku kiingilio kikiwa Tsh.5000 tu.



No comments:

Post a Comment