PATA MATUKIO MBALI MBALI YA KIJAMII POPOTE ULIPO!

Wednesday, September 29, 2010

Mwenyekiti wa kijiji kortini kwa kubaka mwanafunzi


Naibu Waziri wa Elimu nchini,Mwantum Maiza.

MWENYEKITI wa Serikali ya Kijiji cha Makongoro A Wilayani Bunda mkoani Mara, Abdul Masenza Mtahima (56), jana amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Bunda, akikabiliwa na shitaka la kubaka mwanafunzi wa shule ya sekondari Makongoro.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Joackim Tiganga ilidaiwa mahakamani hapo na mwendesha mashitaka wa polisi, Hamza Mdogwa  mnamo Septemba 24, mwaka huu majira ya saa 4 usiku katika kijiji cha Nyamuswa, mshitakiwa alimbaka mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 16, anayesoma kidato cha pili na kumsababishia maumivu makali.

Ilidaiwa mwanafunzi huyo, alikuwa akiishi kwa bibi yake na kwamba siku ya tukio bibi yake alikuwa amesafiri, ndipo mwenyekiti huyo alipofika nyumbani hapo na kuingia ndani na kumkuta mwanafunzi huyo akiwa amelala  ghafla alianza kumchania nguo zake za ndani na kuanza kumbaka.

Mwendesha mashitaka huyo aliendelea kuieleza mahakama hiyo, kuwa baada ya kuona ametenda kitendo hicho alimfungia  ndani hadi kesho yake, alipojikongoja kutokana na maumivu aliyokuwa amepata na kwenda kutoa taarifa kwa ndugu zake.

Habari zaidi kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa baada ya kuona hali hiyo, mwenyekiti huyo aliamua kumdanganya mwanafunzi huyo ili ampeleke katika zahanati za kienyeji kwa ajili ya kupata matibabu.
Mshitakiwa huyo, alikana shitaka lake na kupelekwa mahabusu hadi Oktoba 18, mwaka huu kesi yake itakapotajwa tena.

Chanzo vyanzo vya habari.

No comments:

Post a Comment