mlemavu.
SERIKALI imetakiwa kupanga mikakati ya wazi kuhusu kuondoa umaskini kwa watu wenye ulemavu ambao ni maskini kupindukia nchini, kwa kuwashirikisha katika ngazi mbalimbalia za maamuzi.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Khamisi Nyallu, kuwa umefika wakati wa jamii kushirikishwa kikamilifu kwenye vyombo vya maamuzi kuanzia ngazi ya mtaa hadi taifa.
Alisema umefika wakati kwa serikali kutoa tamko juu ya utekelezaji wa mwongozo wa Afrika kuhusu watu wenye ulemavu ambao ulipitishwa na viongozi wa nchi huru za Afrika mwaka 1999, pamoja na upangaji mikakati ya utekelezaji wa Mkataba mpya wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wenye ulemavu.
Kaulimbiu ya mwaka huu ni ‘Tekeleza ahadi: jumuisha masuala ya watu wenye ulemavu kwenye malengo ya maendeleo ya milenia kuelekea mwaka 2015 na kuendelea’. Mgeni rasmi katika sherehe hizo anatarajiwa kuwa Rais Jakaya Kikwete.
No comments:
Post a Comment