Rais Rafael Correa wa Ecuador ameruhusiwa kutoka hospitalini katika mji mkuu wa Quito alikokimbilia kujificha baada ya kushambuliwa kwa gesi ya kutoa machozi na maafisa wa polisi waliokuwa wakiandamana.
Jeshi la nchi lilitumia nguvu kumuokoa rais huyo, na ufyatulianaji wa risasi ulifuatia. Rais huyo alikaribishwa kwa shangwe nje ya kasri lake alikohutubia watu. Aliwaambia kuwa mtu mmoja amethibitishwa kufariki katika tukio hilo na kuitaja siku hii kama siku ya huzuni kwa nchi hiyo.Makamanda wakuu wa jeshi la Ecuador wametangaza kumuunga mkono rais Correa.
Hisani
Wakati huo huo, muungano wamataifa ya America UNASUR, uliitisha mkutano wa dharura katika mji mkuu wa Argentina Buenos Aries ambapo wametangaza kumuunga mkono rais Correa.Rais wa Peru Alan Garcia amesema kuwa ni jambo la aibu kuwa maafisa wa polisi walijaribu kutumia nguvu kuhujumu uongozi wa kidemokrasia. Amesema kuwa muungano huo utafanya kila juhudi kuimarish auongozi wa rais Correa.
UNASUR imesema kuwa Amerika haitakubali serikali za kidemokrasia kuvunjwa na watu wachache wanaotetea maslahi zao za kibinafsi.
No comments:
Post a Comment