PATA MATUKIO MBALI MBALI YA KIJAMII POPOTE ULIPO!

Friday, October 1, 2010

UMOJA WA MATAIFA WATOA RIPOTI YA CONGO

 

Wakimbizi kutoka Rwanda wakipita Zaire

Umoja wa Mataifa unatarajia kuchapisha ripoti yenye utata juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika miaka ya 90.
Lugha iliyotumika kwenye nakala ya mwisho inaaminiwa kupunguzwa makali baada ya ile iliyotolewa awali bila kutarajiwa kuibua hasira kutoka nchi za Uganda na Rwanda.
Nchi zote mbili zilishutumiwa kwa kuhusika na uhalifu wa kivita dhidi ya Wahutu huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakati wa ghasia hizo.
Walitishia kuondoa majeshi yao ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa.
Ripoti hiyo inayohusu mgogoro kati ya mwaka 1993 na 2003 inaaminiwa kuwa na maelezo ya uhalifu ambayo hayakuwahi kuandikwa hapo awali.
Imezungumzia matukio takriban 600 ikiwemo madai ya mauaji ya raia, utesaji, na uharibifu wa miundo mbinu iliyosababisha vifo vya raia.
Rwanda ilihamaki sana juu ya madai kuwa jeshi lake linaloongozwa na Watutsi huenda lilihusika na mauaji ya kimbari huko Congo, wakati huo ikijulikana kama Zaire mpaka mwaka 1997, dhidi ya Wahutu kutoka Rwanda.
Waandishi wanasema madai ya mauaji ya kimbari dhidi ya serikali ya Rwanda ya sasa, inayoongozwa na Rais Paul Kagame, ni suala tete, kwani anajiwakilisha kama mtu aliyeweza kuyamaliza mauaji hayo ya Watutsi wenzake na Wahutu wenye msimamo wa kati mwaka 1994.
Baadhi ya wapiganaji wanaohusishwa na mauaji hayo walikimbilia Zaire.
Lakini ripoti ya Umoja wa Mataifa inawashutumu kwa kuwaua maelfu ya raia wa Kihutu, waliokimbia na wapiganaji hao.

No comments:

Post a Comment