CHAMA cha Msalaba Mwekundu nchini kupitia kikosi chake maalumu cha Uokoaji na Maafa Mkoa wa Dar es Salaam (Action Team) kimejipanga kuhakikisha kinatoa huduma ya kwanza na dharura kwa kiwango cha juu siku ya uchaguzi.
Mwenyekiti wa Chama cha Msalaba Mwekundu Mkoa wa Dar es Salaam , Mayasa Mikidadi, alieleza hayo jana jijini Dra es Salaam muda mfupi baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa viongozi wapya wa kikosi hicho.
Alisema chama hicho imejiandaa vya kutosha kutoa huduma ya kwanza na ya dharura siku ya kupiga kura na matatizo yote ya dharura.
“Ni hakika kazi iliyopo mbele yetu ni ngumu, lakini hakika uwezo tunao na tutaifanya kwa nguvu zote ili kuhakikisha kila Mtanzania anapata haki ya kupiga kura kwa usalama,” alisema Mayasa.
Aliendelea kusema kikosi hicho kitafanya shughuli za uokoji siku hiyo ambazo zitawalenga watu watakao kuwa wamezidiwa katika foleni, wagonjwa pamoja na kuwasaidia walemavu wa aina yote kusaidiwa kwa lolote litakalotokea wakati wa upigaji wa kura hizo.
Aidha, katika uchaguzi huo, viongozi waliokuwapo kwa muda wa miaka kadhaa walijiuzulu na kupisha uongozi mpya, ambao ulifanywa kwa njia ya amani, huku wakichaguana kwa kanuni ya kupiga kura.
Viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi huo ni pamoja na Dk. Suphian Juma (Kamanda Mkuu), Feruzi Mpili (Kamanda Msaidizi), huku nafasi ya katibu ikichukuliwa na Amina Mwalimu.
Uongozi huo mpya ulishukuru kwa kuchaguliwa kwao kutokana na kuwa na imani nao huku kuahidi kushirikiana bega kwa bega na wanachama wa matawi yote mkoani hapo.
Kwa upande wake Kamanda mpya, Dk. Suphian, aliwashukuru wanachama wote kwa kumchagua huku akiwataka kila mwanachama kushirikiana bega kwa bega ili kufanikisha uongozi makini.
Katika uongozi huo, pia ulisimamiwa na Mratibu wa Mkoa wa chama hicho, Grace Mawala pamoja na Mwekiti wa Wilaya,Dr Mambo
No comments:
Post a Comment