PATA MATUKIO MBALI MBALI YA KIJAMII POPOTE ULIPO!

Sunday, October 17, 2010

WATOTO TUPO LAKINI HAWAJATUONA...!

Nasema ni lazima Jamii isikilize kilio chetu!                   Serikali  iweke mkwazo  na kipaombele 'HAKIMTOTO'
(Nimka Lameck, akisisitiza jambo kwa umati wa wananchi waliojitokeza katika moja ya kampeni jijini Dar es Salaam, ..."Ni hakika katika kutafuta HAKIMTOTO' hakiangaliwi chama, bali tunataka HAKI ipatikane ilikuleta maendeleo yetu"
{NIMKA LAMECK 11yrs, Ni Mwenyekiti wa Chipukizi Wilaya ya Kinondoni na pia ni Mwanaharakati wa kutetea HAKI za watoto nchini}

Furahaaaaa!
Siku zote watoto wanatakiwa kuwa na Uhuru kama huu...wapewe muda na nafasi ya kufanya yale yaliyomema kulingana na wakati wao.

Ni HAKI ya mtoto kuakikisha anapata wasaha wa kucheza michezo ya aina yote akiwa chini ya uangalizi wa wazazi wake ama watu wa karibu.


...Msaada zaidi hata katika hali hii, bado ana HAKI ya kusaidiwa kwa kila jambo..

Walindwe kwa kila hali ilikuepuka vitendo vya jamii hisiyo makini..kuwafanyia vitendo vya kihivu ambavyo  watoto wengi wanafanyiwa hivyo kama inavyolipotiwa mara kwa mara.
Baadhi ya watoto wakiwa wametoka umbali mrefu kutafuta maji ya kunywa.. hata hivyo asilimia ya maji hayo si salama kwa afya zao licha ya kuyapata umbali mrefu...Hii ni moja ya maeneo ya mikoa ya Pwani nchini Tanzania.

HAKIMTOTO, ambayo iliweza kuwa sambamba katika maeneo mbalimbali ya baadhi ya mikoa iliweza kuona hali hiyo na ipo katika mikakati ya kusaidia hali hii.CHUKUA ATUA!

Michezo ni HAKIMTOTO!
Michezo ni moja ya Hali ambayo inafanya watoto kuwa katika hali ya ukaribu na kuacha mambo mabaya ambayo yanapelekea mmong'onyoko wa maadili. mpe nafasi MTOTO ilikutekeleza majukumu yake..


...Hata hali hii inawezekana kuisha kabisa! kama hatua za haraka ambazo viongozi wetu wanaziahidi kuzitekeleza bila vikwazo
Baadhi ya WATOTO wakiwa katika moja ya maeneo ya kujisomea (darasa) moja ya mikoa ya nchini Tanzania...Viongozi wetu muliokatika kampeni kumbukeni HAKIMTOTO ilikutekeleza kwa vitendo na si kuishia kushangiliwa majukwaani na watu wakubwa ambao ....TUNATAKAHAKI!



...Uangalizi thabiti ndiyo nguzo ya ukuaji wa watoto nchini  na sehemu yote duniani.
Watoto walindwe...mazingira kama haya ni hatari  wanapata matatizo mbalimbali sambamba na magonjwa ambukizi ambayo kwa hali halisi ya Mtanzania wa kawaida ni hatari


...Maombi  kutumikia katika Dini ni  HAKIMTOTO!
Kila mzazi anatakiwa kumsaidia mtoto na kumpa uhuru mtoto kutumikia hali ya kiimani iliyosahihi na imara kwa misingi yake..

Mdau wa Blog ya HAKIMTOTO, unaombwa kutuma picha na taarifa mbalimbali ambazo zinahusu watoto nchini kokote pale Duniani.
Tuma ; Email; nimkalameck@yahoo.com/+255719076376




No comments:

Post a Comment