PATA MATUKIO MBALI MBALI YA KIJAMII POPOTE ULIPO!

Monday, November 8, 2010

SHELISHELI,TANZANIA KUKUZA UTALII


Sauda Kilumanga wa kwanza kushoto akiwa na Balozi wa Heshima wa visiwa vya Shelisheli nchini, Maryvonne Pool akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari mapema leo wakati akiongea juu ya onyesho la Visiwa hivyo na Tanzania litakalofanyika Novemba 15 hadi 20, kulia kwake ni Mkuu wa Protocal Helen Sweya.

VISIWA vya Shelisheli kwa kushirikiana na Tanzania vina mpango wa kuendeleza utalii wa ndani na nje kupitia wiki ya maonyesho ya vitu mbalimbali itakayoanza Novemba 15 hadi 20, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam, Balozi wa Heshima wa visiwa hivyo nchini, Maryvonne Pool, alisema maonyesho hayo yatakuza mahusiano ya karibu baina ya Tanzania na Shelisheli.

Alisema kwa kuwa uchumi wa Tanzania na Shelisheli umekuwa kwa kiwango kikubwa kupitia nyanja za utalii wa ndani na nje, hivyo ni vema watu wakajitokeza katika maonyesho hayo.

“Lengo ni kukuza uchumi hususan nyanja ya utalii baina ya nchi hizi mbili, hivyo wadau mbalimbali watajumuika pamoja na kushuhudia vitu mbalimbali vya Shelisheli vitakavyokuwa vikionyeshwa.

“Pia watajifunza pamoja na kupatiwa ujuzi wa jinsi visiwa hivyo vilivyofanikiwa kiuchumi kupitia utalii,” alisema Maryvonne.

Katika wiki hiyo maonyesho mbalimbali yakiwemo ya vyakula vya watu wa visiwa vya Shelisheli vitaonyeshwa.

Kwa upande wake Helen Sweya Mkuu wa onyesho hilo, alisema uchumi wa Shelisheli ambao asilimia kubwa umetokana na utalii wa ndani, utaleta chachu na kwa wawekezaji wa nje kuijua Tanzania na kuongeza ukuaji wa uchumi.

“Wengi wanaijua Shelisheli hivyo kwa kufanyika nchini Tanzania watapata kufursa ya kujitangaza zaidi,” alisema Sweya.

No comments:

Post a Comment