PATA MATUKIO MBALI MBALI YA KIJAMII POPOTE ULIPO!

Wednesday, January 19, 2011

MABALOZI WA MALARIA WATAKIWA KUTUMIA MBINU MPYA



 Mabalozi wa Malarai, ambao ni wasanii nchini Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na waziri wa Afya na Ustawi wa jamii mapema leo walipotembelaea wizarani hapo.



WAZIRI wa Afya, Dk. Haji Mponda, ametoa rai kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya ambao pia ni mabalozi wa mradi wa kupambana na ugonjwa wa malaria wa Zinduka, ‘Malaria No More’ kutunga nyimbo zitakazoleta hamasa ya kubadili tabia iliyojengeka miongoni mwa jamii ya kuudharau ugonjwa huo.

Mponda alisema kwamba wasanii hao watafute njia mpya ya kusambaza ujumbe kutokana na tabia iliyojengeka miongoni mwa watu wengi kudharau kujitibu malaria, ugonjwa ambao unaua kwa haraka zaidi hasa wanawake na watoto.

“Utaona mama anaona mtoto ana dalili zote za malaria, lakini atakachofanya ni kumpatia dawa za kutuliza maumivu na kuendelea na shughuli zake, kadhalika kwa vijana wenzenu, nao wanaoongoza kwa kudharau, utakuta mtu akijisikia ana dalili zote za malaria atapata kinywaji chake na kwenda zake, tofauti akiwa anasumbuliwa na magonjwa kama kaswende, hapo atajitibu kwa haraka zaidi,” alisema waziri.

Wakati huo huo, Profesa Jay akizungumza kwa niaba ya wasanii wengine, alimwomba waziri kufanya nao kazi pamoja katika utekelezaji wa majukumu yao, ombi lililokubaliwa.
Kundi hilo la mabalozi wa malaria ambalo lilikwenda kumtembelea waziri ofisini kwake jana, linaundwa na Profesa Jay, Lady Jaydee, Fid Q, Barnaba, Marlow, Mwasiti, Diamond, Amini, Banana na B Twelve.

No comments:

Post a Comment