Liu Xinsheng
JESHI la Wanamaji wa China (PLA) linatarajia kutoa huduma ya dawa bure katika bandari ya Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Jamhuri ya Watu wa China.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara Habari (MAELEZO) mapema leo jijini Dar es Salaam, Balozi wa China nchini, Liu Xinsheng, alisema huduma hiyo itatolewa kati ya Oktoba 19-24 na kwamba lengo ni kufahamu kama watu wanahitaji msaada huo ili kuweza kutibu magonjwa mbalimbali kwa nchi za Afrika.
Alisema hii ni mara ya tatu kutoa huduma kama hiyo nchini na kuongeza kuwa meli hiyo imeshapita katika nchi za Djibouti na Kenya kabla ya kupita visiwa vya Shelisheli na Bangladesh.
Balozi huyo alisema meli hiyo ambayo imeshawasili imechukua magari ya wagonjwa 300, vitanda vya hospitali 450, madaktari na wauguzi 2414.
Alisema, timu ya madaktari kutoka meli hiyo itapelekwa katika shule za msingi kwa ajili ya kuwachunguza macho na kutoa matibabu.
No comments:
Post a Comment