PATA MATUKIO MBALI MBALI YA KIJAMII POPOTE ULIPO!

Saturday, October 16, 2010

SERIKALI YA TANZANIA IJULISHE UMMA HAKI ZA WATOTO !

Watoto ni Hazina! Kila jambo wanatakiwa kushirikishwa ..

Karibu nchi nyingi Dunia wanajari Haki za watoto kwa asilimia kubwa kutokana na misingi thabiti waliyojiwekea muda mrefu! Ni hakika Tanzania mbali na kuwa na amani tuliyonayo kwa muda mrefu, kumejitokeza hali ya uvunjwaji wa 'HAKIMTOTO' hii ni kwa kufanyiwa vitendo vya kikatili kila siku hapa nchini.

...Mimi Nimka Lameck, Mwenyekiti wa Chipukizi Wilaya ya Kinondoni na Mwanaharakati wa kutetea Haki za watoto nchini, pamoja na mradi maalum ambao unatalajia kuanza hivi punde wa 'HAKIMTOTO', Natoa tamko na angalizo juu ya hali hii ya uvunjikaji wa HAKI zetu ambazo tunafanyiwa sisi watoto kila kukicha.

Jamii na Serikali kwa kushirikiana na taasisis zingine ziwajali watoto ikiwemo kufundisha HAKIMTOTO kila kona kama yalivyokuwa matangazo ya biashara hapa nchini.
...Watoto wengi wanafanyiwa vitendo vya ajabu na ndugu zao,watu baki pamoja na kutumikishwa kwa ujila mdogo.

Asilimia 66.8 watoto wengi wanafanyiwa vitendo vya kikatili na ndugu zao
Asilimia 51.5 watoto wanafanyiwa vitendo vya kikatili na watu baki
Asilimia 2.7 watoto wanafanyiwa vitendo vya kikatili na watu waliokuwa katika taasisi za umma/Serikali na makundi maalum kwa Taifa.
Kwa takwimu hizi zaidi zitaendelea kutolewa hapo baadae..ama kama unatakwimu zingine zaidi unaweza kuwasiliana kupitia; Email; nimkalameck@yahoo.com/+255719076376

No comments:

Post a Comment